Ajenda Ya Maendeleo Mapya Ya Umoja Wa Mataifa Inateua Wajibu Mpya kwa Vijana
Na Rodney Reynolds
UMOJA WA MATAIFA (IDN) – Katibu Mkuu Ban Ki-moon, ambaye ameendelea kusisitiza jukumu muhimu kushughulikiwa na vijana katika utekelezaji wa Malengo Endelevu ya Maendeleo (MEM) ya 17 ya Umoja wa Mataifa ifikapo mwaka wa 2030, anasema kuwa vijana wengi duniani kote wamekuwa wakiathiriwa na migogoro ya kiuchumu na kushuka kwa uchumi.
“Kama viongozi wa tochi wa ajenda ya maendeleo mapya, mna jukumu muhimu kushughulikia katika kukomesha umaskini, kukosekana kwa usawa, njaa na uharibifu wa mazingira. Hatua zenu zitakuwa katikati katika kukaribisha kipindi ambapo hakuna mtu anaachwa nyuma,” aliambia mkutano wa vijana.…