Mradi wa Kihistoria Unakusudia Upanzi wa Miti nchini Togo – Fursa za Mapato kwa Wanawake
Na Ramesh Jaura
BERLIN | TOKYO (IDN) – Togo iliyoko Afrika Magharibi ni mahali pa mradi wa hatua muhimu kati ya Soka Gakkai, shirika la jamii ya kimataifa ya Wabudha na Shirika la Kimataifa la Mbao za Kitropiki (ITTO). Mashirika hayo mawili yametia saini memoranda ya kuzindua mradi wa upanzi wa miti unaotoa fursa za mapato kwa vikundi vya wanawake katika maeneo mawili ya vijijini nchini Togo.
Memoranda inayohusisha mchango wa yen milioni 10 (Dola za Marekani 93,300) kwa awamu ya kwanza ya mwaka mmoja ya mradi huo ilisainiwa mnamo Julai tarehe 1 katika makao makuu ya Soka Gakkai (SG) huko Tokyo. Mradi utaanza Septemba tarehe 1.…