Wahandisi wa Nishati ya Jua wa Kike Wanatoa Mwangaza katika Vijiji vya Mbali kule Zanzibar
Na Kizito Makoye
KENDWA, Tanzania (IDN) – Giza linapoingia, Natasha Mahmood na kaka yake hupiga gumzo karibu na mwali wa taa ya mafuta taa, wakiharakisha kumaliza kazi yao ya ziada kabla mama yao aizime taa ili kuhifadhi mafuta.
“Mimi mara nyingi hujaribu kuikamilisha mapema. Lakini hilo sio suala wakati wote. Mwalimu wangu wakati mwingine huniadhibu kwa ajili ya kushindwa kukamilisha kazi yangu,” anasema Mahmood, moshi kutoka kwenye taa unapofuka ndani ya paa la mabati lililochafuliwa na masizi yanayotokana na moshi.…